<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><hymn_number>46</hymn_number>
<title>Twae Wangu Uzima TZR46</title>
<lyrics>[V1]
 Twae wangu uzima,
 Sadaka ya daima;
 Twae saa na siku,
 Zikutukuze huku.

[V2]
 Twae mikono nayo
 Ifanye upendavyo,
 Twae yangu miguu
 Kwa wongozi wako tu.

[V3]
 Twae sauti yangu,
 Niimbe kwa Mungu tu;
 Itwae na midomo,
 Ijae neno lako.

[V4]
 Twae dhanabu pia,
 Na yote ya dunia;
 Twae yangu hekima,
 Upendavyo tumia.

[V5]
 Nia itwae, Mungu,
 Haitakuwa yangu;
 Twae moyo; ni wako,
 Uwe makazi yako.

[V6]
 Twae mapenzi yangu,
 Sifa za moyo wangu;
 Twae kabisa nafsi
 Nniwe wako halisi.</lyrics>
</song>